Local Bulletins

MWANAUME MMOJA AFIKISHWA MAHAKAMA YA MARSABIT KWA KOSA LA KUMNAJISI MTOTO NA KUMPA MIMBA.

Na Caroline Waforo

Mwanaume moja mwenye umri wa miaka 24 alifikishwa mahakama ya Marsabit Ijumaa kwa kosa la kumnajisi msichana wa miaka 14 na kumpachika mimba.

Ni kitendo ambacho kinaripotiwa kufanyika katika eneo la loiyangalani eneo bunge la laisamis, kaunti ya Marsabit, kati ya mwezi January na February mwaka huu.

Mtuhumiwa Wario Namana alifikishwa katika mahakama ya marsabit mbele ya hakimu SK Arome ambapo pia ameshtakiwa kwa kosa la pili la kuhusika katika kitendo cha aibu.

Alikana mashtaka yote mawili na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000 au kiwango sawia pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 13 mwezi Juni 2024 na kusikilizwa tarehe 14 mwezi uo huo.

Subscribe to eNewsletter