Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
NA CAROL WAFORO
Mtu mmoja amethibitishwa kufariki dunia katika mgodi wa Hillo ulioko eneo la Dabel eneobunge la Moyale.
Akithibitisha kisa hicho afisa wa upelelelezi kaunti ya Marsabit Luka Tumbo amedokeza kuwa maafisa wa polisi waliwafurusha wachimba migodi kutoka machimbo hayo mapema Jumanne asubuhi.
Katika harakati hiyo watu 34 raia wa Kenya na Ethiopia walikamatwa.
Wachimba migodi walijaribu kuwaokoa wenzao na katika makabiliano hayo huku moja wa wachimba migodi akipata majeraha mabaya na kufariki dunia wakati akipokea matibabu katika hospitali ya Moyale.
Jamaa huyo ni raia wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 19.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya idara ya usalama hapa Marsabit kuongeza kikosi cha maafisa wanaoshika doria katika machimbo hayo na kuwaondoa maafisa waliokuwa wakishika doria hapo awali.
Hata hivyo duru zinaarifu kuwa ni watu wawili ndio waliofariki kwenye makabiliano hayo japo DCI imedhibitisha kifo cha mtu aliyeaga dunia hospitalini pekee.