Local Bulletins

MTU MMOJA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MOJA KWA KOSA LA KUIBA VITU VYENYE DHAMANI YA SHILLINGI 150,000 MALI YA KAMPUNI YA MEISO.

NA GRACE GUMATO

Mwananume mmoja mwenye umri wa makamu amefikishwa katika Mahakama Ya Marsabit  hii leo kwa kosa  la wizi.

Mshukiwa Ibrahim Yayo Yede anadaiwa kwamba kati ya tarehe 3 na 4 mwezi huu ktk mtaa wa Marsabit aliweza kuiba vitu vyenye dhamani ya shillingi 150,000 mali ya kampuni ya MEISO kwa kuvunja dirisha na kuharibu gari la kampuni hiyo.

Mshukiwa alifikishwa mbele ya hakimu mkaazi Simon Arome na kukubali mashtaka dhidi yake huku mahakama ikimpa kifungo cha mwaka moja gerezani au faini ya shillingi 150,000.

Wakati huo huo Hussein Barowa alifikishwa mbele ya mahakama ya Marsabit hii leo kwa kosa la kupiga na kuumiza mtu ambayo ni kinyume na sheria

Mshukiwa  mnamo terehe 9 mwezi huu katika eneo la Maikona kaunti ndogo ya Northhorr anadaiwa kupiga na kumuumiza mlalamishi Jaldo Bagaja na kumpa majeraha mabaya.

Mshukiwa alifikishwa mbele ya hakimu mkaazi Simon Arome na kukubali kesi dhidi yake huku mahakama akimpa kifungu ya mwaka moja gerezani.

……………………….

Subscribe to eNewsletter