Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na JB Nateleng,
Mkurugenzi wa programu katika shirika lisilo la kiserikali la Pastrol People Initiative Steve Baselle amesema kuwa shirika hilo litaandaa mswada wa kupeleka bungeni ili kuweza kuhoji serekali kuhusu upatikanaji wa taka za nyuklia katika wadi ya Kargi eneo bunge la Laisamis Kaunti ya Marsabit.
Baselle ameelezea kuwa ni haki ya wakazi wa kargi kuelezewa kuhusu nyuklia ambayo serekali inadaiwa kutupa katika eneo hilo ambayo kwa muda sasa umewafanya wengi kuweza kuugua ugonjwa wa saratani na wengine kupoteza wapendwa wao.
Kulingana na Basele ni kuwa jambo hilo linakiuka haki za kibinadamu hivyo kutaka serekali kuchukua jukumu la kuhakikisha kuwa haki ya wakazi wa Kargi linapatikana.
Baselle ameitaka serekali kufichua ni maeneo yepi ambayo taka hizo za nyuklia ziliweza kuzibwa na pia kupeana mwelekeo wa kuilinda eneo hilo kwa manufaa ya wakazi wa Kargi, ambao wanasema kuwa miaka 36 zilizopita kulikuweko na zoezi la uchimbaji mafuta katika eneo hilo.
Kadhalika baselle amechangamoto serekali kuweza kuwafidia wale ambao walipoteza wapendwa wao kwani ni jambo la kusikitisha kuona wakazi hawa waking`ang`ana kutafuta fedha za kupeleka wapendwa wao hospitali na baadae kuambulia patupu kwa kupoteza wapendwa wao pamoja na fedha hizo hivo kubakia maskini wasijue la kufanya.