Local Bulletins

MSINGI WA MAENDELEO NI ELIMU – WAZIRI WA ELIMU WA MARSABIT

NA SILVIO NANGORI

Waziri wa Elimu wa Kaunti ya Marsabit,Bi. Ambaro Abdulah Ali, amesisitiza kuwa elimu ndiyo msingi wa maendeleo katika kaunti hiyo. Akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa shule ya upili ya wasichana ya Kulal, katika wadi ya Loyangalani, Waziri Ambaro amewataka wananchi kuelewa umuhimu wa elimu na kuwapeleka watoto wao shuleni ili wafaulu maishani.

Aidha, Waziri Ambaro amewaita wananchi wa Marsabit kuasi mila potovu ambazo zimekuwa zikiwarudisha nyuma. Kauli hii imeongezewa uzito na mwakilishi wa wadi ya Loyangalani, Musa Emojo, ambaye amesema kuwa ujenzi wa shule hii ya upili ya wasichana umesababisha mabadiliko makubwa katika jamii inayoishi Loyangalani.

Emojo amewapongeza waanzilishi wa shule hii na kuwataka wananchi kutokubali ukabila na badala yake kukumbatia ushirikiano wa pamoja ili kuharakisha maendeleo.

Subscribe to eNewsletter