Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Grace Gumato
Mshukiwa anayedaiwa kupora dula la jumla la Basmart mjini Marsabit amefikishwa katika mahahakama ya marsabit hii leo kwa kosa la wizi wa kimabavu.
Mshukiwa Hendry Halkana George anadaiwa kuwa mnamo tarehe 6 mwezi huu katika duka la jumla la Basmart iliyoko katika mtaa ya saku kaunti ya Marsabit yeye pamoja na wengine ambao hakuwa mbele ya mahakama waliiba shillingi 30,000 kwa kutumia bunduki.
Mshukiwa alifikishwa mbele ya hakimu mkuu Christine Wekesa na kukana mashtaka dhidi yake huku mshukiwa akilalamika kuwa alipigwa na kuumizwa na maafisa wa polisi akiomba mahakama apelekwe hospitali ili apate matibabu huku mahakama ikimpa ruhusa ya kupelekwa hospitali hata hivyo mahakama alimwachilia kwa bondi ya shilling 30,000 na pesa taslimu 100,000.
kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena tarehe 6 mwezi ujao na kusikilizwa terehe 20 mwezi ujao.
Wakati huu uo Abdulahi Golo amefikishwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kitishia kuua.
Mshukiwa anadaiwa kuwa mnamo kati ya tarehe 4 na 5 mwezi huu katika eneo la Manyatta Ote Kaunti Ya Marsabit alitumia maneno ya kutishia kuua mlalamishi Daka Miyo.
Mshukiwa alifikishwa mbele ya hakimu mkuu Christine Wekesa na kukubali mshataka dhidi yake huku kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa tena tarehe 24 mwezi huu….