Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Isaac Waihenya,
Serekali ya kaunti ya Marsabit imekanusha madai kuwa ilihusika katika kukamatwa kwa Seneta wa kaunti ya Marsabit Mohamed Chute na tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC.
Kwa mujibu wa msemaji wa serekali ya kaunti ya Marsabit Abdub Barille ni kuwa serekali ya kaunti haukuhusika kwa vyovyote vile na madai ya ufisadi yaliyoibuliwa EACC kuhusiana na Seneta Chute na badala kusifia hatua hiyo huku akitaja kwmaba ipo hoja ya Seneta pia kuchunguzwa mienendo yake.
Akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, Barille amemtaka Seneta Chute kuubebe msalaba wake haswa katika maswala nayohusiana na uadilifu.
Barille hata hivyo ameweka wazi kwamba juhudi za kuweza kuwapatanisha Senata Chute na Gavana Mohamud Ali zimekuwa zikifeli kutokana na masharti kamali ambayo hutolewa na Seneta.
Barille amefichua kwamba mbunge wa Saku Dido Ali Rasso ndie amekuwa akimtumia Seneta Chute ili kulemaza utendakazi wa serekali ya kaunti.
Hata hivyo msemaji wa serekali Abdub Barille amekosoa pia utendakazi wa vyombo vya habari hapa jimboni Marsabit huku akiwataja kwamba serekali ya kaunti pio tayari Kuandaa mkao naoi li kutatua tofauti zilizopo.
Onyo kali latolewa kwa wanafanya biashara ya kuuza migadarati hapa jimboni Marsabit
Idara ya watoto katika kaunti ya Marsabit wazazi kuwajibika zaidi katika malezi ili kusaidia katika kupambana na utumizi wa mihadarati.
Kwa mujibu wa afisa wa watoto katika kaunti ya Marsabit Abudo Roba ni kuwa ni jukumu la kila mmoja katika jamii na haswa wazazi kuhakikisha kwamba watoto wachanga hawajiingizi katika utumizi wa mihadarati.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini mwake, Roba ametaja kwamba ni jambo la kuhuzunisha mno kuona kwamba watoto wadogo wa hadi gredi ya 3 wanavuta bangi.
Akirejelea kisa cha siku ya jumatatu wiki hii ambapo vijana watano wa kati ya umri wa miaka 9 hadi 11 katika mojawepo ya shule za msingi hapa mjini Marsabit walipatikana wakivuta bangi, Roba amewaonya wote wanaofanya biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya huku akiweka wazi kwamba yeyote atakayepatikana akiendeleza biashara hiyo atachuliwa hatua kali za kisheria.
Ameahidi kuwa watashirikiana na walimu pamoja na wazazi ili kuhakikisha kwamba watoto waliotolewa mitaani hawawafunzi wenzao utovu wa nidhamu.