Wakazi wa vijiji vya Nawapa,Kulamawe na Kilimambogo Loiyangalani,wamelalamikia uhaba wa maji…
January 15, 2025
Huku wito ukizidi kutolewa dhidi ya dhulma za kijinsia jamii za kaunti ya Marsabit zimetakiwa kuasi ndoa za mapema na ukeketaji miongoni mwa wasichana.
Akizungumza kwenye hafla ya kufuzu kwa wasichana waliopokea mafunzo katika programu ya Gaddis Gamme mke wa Gavana wa Marsabit Alamitu Jatani amesema kuwa mila na tamaduni za Marsabit ni nzuri ila kuna badhi ya mambo yaliyopitwa na wakati.
Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya Loglogo Rose …. ametaja mimba ya mapema kama moja ya changamoto wanayokumbana nayo kama jamii zinazoishi katika kaunti ndogo ya Laisamis
Hata hivyo Fatuma Leruk aliyezungumza kwa niaba ya wazazi wengine amemshukuru programu hiyo ya kufunza wasichana iliyoasisiwa na Alamitu huku akitaka wanafunzi walionufaika kuwafunza wenzao waliokosa fursa hiyo adimu.
Aidha Wasichana walionufaika na mafunzo hayo ya siku tano wamesema kuwa wamefaidika pakubwa na kuahidi kueneza ujumbe waliopata kwa wasichana wengine waliokosa kuhudhuria mafunzo hayo.