Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Mila Potovu zimetajwa kama sababu kuu zinazochangia visa vya dhulma za kijinsia hapa nchini.
Kwa mujibu wa afisa wa jinsia katika serekali ya kaunti ya Marsabit Joshua Loitoro ni kuwa japo kuna mila nzuri ambazo zinafaa kuenziwa ila baadhi za mila hapa jimboni Marsabit zimekuwa zikirejesha nyuma hatua ambazo zimepigwa katika kukabiliana na dhulma za kijinsia.
Loitoro ametoa wito kwa wakaazi wa Marsabit kushirikiana na serekali pamoja na mashirika yasiyoyakiserekali katika kufaulisha vita dhidi ya dhulma za kijinsia.
Aidha Loitoro amesifia hatua ambazo zimepigwa na mashirika ya kijamii katika kuhakikisha kwamba wananchi wanapata hamasa.