ULIMWENGU WAADHIMISHA SIKU YA WALEMAVU JANA,HUKU WITO WA KUWAPELEKA WATOTO WALEMAVU SHULENI UKISHEHENI…
December 4, 2024
Michezo ndio nguzo ya kuwauunganisha vijana na kuleta Amani katika jimbo la Marsabit.
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa shirika la REPAL Eddie Lemoile.
Akizungumza na idhaa hii, wakati wa mashindano ya mchezo wa voliboli ulioandaliwa katika chuo cha anuwai cha Don Bosco mjini Marsabit, ambayo ilifadhiliwa na shirika la REPAL, Lemoile amesema kuwa vijana wanapaswa kuhusishwa msimu huu wa likizo kwa kuandaa michuano kama hiyo, kwa sababu kupitia mashindano vijana wanapata fursa ya kufahamiana na kuelewana hivyo kudumisha Amani.
Lemoile amewataka vijana jimboni Marsabit kukumbatia mchezo wa voliboili akidai kuwa ni rahisi kuelewa zaidi ikilinganisha na michezo mingine.
Lemoile amesema kuwa shirika la REPAL litazidi kuwasaidia vijana kuweza kutambua talanta zao kwa ajili ya kuboresha jamii na vizazi vijavyo jambo analosema litasaidia kudumisha uwiano kati ya jamii za jimboni la Marsabit.
Wakati huo huo, Vijana waliohusika katika michuano hiyo wamesifia hatua hiyo wakisema kuwa imewafanya kutangamana na wenzao kutoka maeneo tofauti hivyo kuwasadia kujijenga kimaadili na pia kuwafanya kuunda urafiki utakaosaida katika kudumisha Amani.
Vijana hawa wameirai serekali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserekali kuweza kushirikiana na shirika la REPAL kupanga michuano kama hiyo jimboni, ili kuwafanya vijana kutambua na kuenzi talanta zao.