Local Bulletins

MGOMO WA KUPPET KUENDELEA LICHA YA MAHAKAMA KUTUPILIA MBALI MGOMO HUO KWA MUDA.

Na Samuel Kosgei

CHAMA cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini (KUPPET) kimeshikilia kuwa mgomo wa walimu bado upo na utaendelea licha ya uamuzi wa mahakama kuwa mgomo huo unafaa kusimamishwa hadi keshi iliyowasilishwa isikilizwe na kuamuliwa na mahakama hiyo.

Katibu wa chama cha KUPPET kaunti ya Marsabit Sarr Galgalo akizungumza na idhaa hii amesema kuwa chama chao kupitia katibu mkuu wao Akello Misori amesema kuwa walimu wao hawarejei kazini kwani mwajiri wao TSC kwa muda mrefu haijakuwa ikiheshimu mahakama pia.

Anasema kuwa mgomo wao ni halali na wanapanga kufanya maandamano makubwa ya walimu kote nchini.

Wakati uo huo ameshutumu tume ya kuajiri walimu TSC kwa kutishia walimu wa sekondari msingi JSS. Sarr anasema walimu wa JSS ni walimu walio chini ya muungano wao wa KUPPET.

Aidha ametaka walimu wakuu wa shule za sekondari marsabit kutotishia walimu ambao ambao hawajaripoti shuleni kwa kuwa wanapigania haki zao pia kwenye mgomo ambao unaendelea kwa sasa.

Subscribe to eNewsletter