Watu 25 ikiwemo watoto 6 waendelea kupokea matibabu katika eneo la Kamboe,Marsabit baada ya kudaiwa kula mzoga wa ngamia.
February 25, 2025
Na Caroline Waforo,
Mbunge wa eneo la Northhorr kaunti ya Marsabit Wario Guyo Adhe ni kati ya wabunge kadhaa humu nchini ambao wanaohusishwa na matumizi mabaya ya fedha za hazina ya ustawi wa maeneobunge nchini (NG-CDF).
Hii ni kulingana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali Nancy Gathungu.
Kulinga na ripoti hiyo baadhi ya wanafunzi waliodaiwa kupokea pesa hizo kwa ajili ya masomo hawawezi kutambulika.
Aidha ripoti hiyo ya Bi. Gathugu imesema kuwa hakuna stakabadhi zilizowasilishwa kuthibitisha kusailiwa kwa wanafunzi kutoka familia zisizojiweza na ambao walinufaika, hali ambayo inaibua wasiwasi.
Wabunge wengine waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi, mbunge wa Saboti Caleb Amisi, yule wa Thika Town Alice Nganga kati ya wengineo.