Local Bulletins

MBUNGE WA MOYALE, ATAKA SERIKALI KUONDOA MARUFUKU YA KUSAKA DHAHABU DABEL

Mbunge wa Moyale, Profesa Guyo Jaldesa, ameitaka serikali kuondoa rasmi tangazo la kufungwa kwa migodi ya dhahabu ya Hillo huko Dabel na kurasimisha kufunguliwa kwake upya.

Mbunge huyo amesema kuwa, licha ya serikali kufunga maeneo hayo kwa muda kupitia tangazo rasmi kwa sababu za usalama, inadaiwa kuwa shughuli za kusaka dhahabu hiyo inaendelezwa kwa njia ya siri na baadhi ya watu huku wakipozwa ulinzi kinyume na sheria.

Profesa Guyo aliteta kuwa hatua hiyo si sawa kwani wenyeji wa eneo hilo wananyimwa fursa ya kuchimba dhahabu ya Dabel ilhali ni rasilimali zao za asili.

Katibu katika wizara ya Madini na Uchumi wa baharini Elijah Mwangi na Gavana wa Marsabit Mohamud Ali Jumatano waliandaa kikao na wakaazi wa eneo hilo kuhusu namna ya kurejesha shughuli za kuchimba tena madini.

Subscribe to eNewsletter