Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Na Caroline Waforo
Marufuku iliyoko katika mgodi wa illo eneo la Dabel eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit itaendelea kutekelezwa.
Haya ni kulingana na waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki ambaye alizungumza katika uzinduzi wa nne wa mpango wastani ambao unajumuisha kipindi cha mwaka 2023-2027, kikao cha kuhusisha umma na ufafanuzi wa programu ya maendeleo katika kaunti ya Marsabit, hafla iliyoandaliwa katika ukumbi wa kanisa katoliki.
Waziri Kindiki alisema kuwa serikali kuu kwa ushirikiano na serikali ya kaunti itaweka mikakati mwafaka ya kuhakkikisha kuwa shughuli zinarejelewa japo kwa utaratibu na hivyo kuzuia maafa.
Aidha ametoa onyo kali Kwa walio na nia ya kuendeleza shughuli katika mgodi huo kinyume na Sheria.