Local Bulletins

MAKUNDI YANAYOFANYA BIASHARA YA UPANZI WA MICHE KAUNTI YA MARSABIT YATAKIWA KUJIANDIKISHA NA IDARA YA MISITU ILI KUNUFAIKA NA MIPANGO YA SEREKALI.

Na Isaac Waihenya,

 Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametakiwa kutunza miche ambayo imepandwa ili kuongezea kiwango cha miti hapa jimboni.

Kulingana wa afisa mkuu katika idara ya misitu na mali asili kaunti ya Marsabit Pauline Marleni aliyeongea na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee,ni kwamba iwapo jamii haitatunza miche iliyopandwa basi juhudi zilipigwa katika zoezi la upanzi wa miche zitaambulia patupu.

Aidha Marleni ameyataka makundi yanayofanya biashara ya upanzi wa miche kujiandikisha na idara ya misitu ili kunufaika na mipango ya serekali.

Marleni amewataka wananchi kuhakikisha kwamba wanapanda miti haswa wakati huu ambapo kunashuhudiwa mvua fupi ili kutimiza malengo ya jimbo ya miche milioni 204 kila mwaka na 2.04 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Subscribe to eNewsletter