Marsabit yatajwa kuwa miongoni mwa kaunti zinazokuwa kwa kasi kimaendeleo.
January 15, 2025
WAMILILIKI na madereva wa magari ya abiria na yale ya kibinafsi wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha ajali haswa katika msimu huu wa sherehe nyingi za mwezi December.
Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Marsabit Central David Saruni akizungumza na meza yetu ya habari amesema kuwa mara nyingi ukosefu wa umakinifu wa madereva huchangia ajali za barabara.
Ametoa wito kwa madereva kuhakikisha magari yao yanafanyiwa ukarabati ya mara kwa mara ili kuzuia ajali hizo.
Wakati uo huo DCC Saruni amesema kuwa idara ya usalama katika kaunti ndogo ya Marsabit Central na jimbo lote kwa ujumla iko macho msimu huu wa sherehe za krismasi.
Anasema maafisa wa wote wa usalama walio kwenye likizo wamerejea kazini ili kushika doria katika sehemu mbalimbali za jimbo.
Saruni pia ameomba wananchi kutumia mvua za sasa kupanda miche ili kutimiza kupanda idadi ya miti iliyopewa jimbo hili na wizara ya mazingira na Tabia Nchi.
Anasema kuwa serikali ina mpangilio kupitia idara ya misitu KFS kupanda miti sehemu mbali mbali kaunti ya Marsabit.