Wakazi wa vijiji vya Nawapa,Kulamawe na Kilimambogo Loiyangalani,wamelalamikia uhaba wa maji…
January 15, 2025
Na huku taifa likijiandaa kuadhimisha siku ya Virusi vya Ukimwi ulimwenguni tarehe 1 mwezi ujao wa Dicemba maambukizi ya virusi hivyo yametajwa kuongeza katika kaunti ya Isiolo.
Haya yalibainishwa na Hadijah Omar ambaye ni mwasisi wa shirika la Pepo La Tuamini Jangwani wakati wa mkutano na makundi 20 yanayofanya kazi kwa ukaribu na shirika hilo katika kuboresha afya vijijini.
Khadija ameitaka jamii haswa vijana kubadili mienendo ambayo inachangia katika ongezeko la virusi hivyo. Kadhalika ameitaka jamii kukomesha unyanyapaa dhidi ya waathiriwa wa virusi hivyo.
Ha hivyo wakaazi waliohudhuria wamepongeza kikao hicho wakisema kuwa kuna haja ya uhamasisho zaidi kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na kutokomeza unyanyapaa.