Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Maafisa wawili wa kitengo cha DCI katika kaunti ya Marsabit wanaguuza majereha ya risasi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kushabuliwa na watu wasio julikana katika Eneo ya Funan Idha iliyoko katika kaunti Ndogo ya Turbi.
Akidhibitisha kisa hiki kwa njia ya simu OCPD wa Turbi Daniel Parmuat ni kuwa mashambulizi hayo yalifanyika saa sita usiku wa kuamkia leo .
Aidha afisa Parmuat amesema kuwa gari lililoshambuliwa lilikuwa na maafisa watatu, huku wawili wakiuguza majeraha na moja wao hajulikani alipo mpaka wakati wa mahojihano na idha hii.
Afisa huyo aidha amesema kuwa afisa mmoja alipigwa risasi tumboni na kichwa ila yupo katika hali nzuri kwa sasa na anapokea matibabu katika hospitali ya Sololo mission.
Hata hivyo Parmuat amseema kwamba uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha tukio hilo.