Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
NA CAROL WAFORO
Na Carol Waforo.
Maafisa wa klinki jimboni Marsabit wanatarajiwa kurejea kazini ifikapo tarehe 1 Agosti 2024.
Hii ni baada yao kuingia kwenye makubaliano ya kurejea kazini na wizara ya afya jimboni Marsabit.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani waziri wa afya Malicha Boru amesema kuwa jana Jumatatu washikadau mbalimbali serikalini waliandaa mkutano na muungano wa maafisa wa kliniki KUCO ambapo waliafikiana makubaliano hayo.
Malicha anasema kwua swala la kucheleweshwa kwa mishahara litaangaziwa huku pia wakikubalina kuwa mshahara wa mwezi Novemba mwaka jana utalipwa kufikia mwishoni mwa mwezi septemba mwaka huu.
Na kwenye swala la kupandishwa vyeo kwa maafisa wa kliniki Malicha amedokeza kuwa hilo litawezekana pindi tu serikali itakapopata fedha haswa kwa waliongeza viwango vya elimu na wanaohitaji kupandishwa vyeo.
Na baada ya maafisa hao wa kliniki kulalama kuhusiana na makato kama vile NHIF, NSSF kutowasilishwa katika taasisi husika, Malicha anasema kwua wataunda jopo kazi ili kuchunguza swala hilo hata katika idara zingine.
Na huku maafisa wa kliniki wakitaka idadi yao kuongezwa Malicha ametupilia mbali uwekezano wa maafisa zaidi kajiriwa katika mwaka huu wa kifedha.