Local Bulletins

KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MAJI SAFI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT

 

BY CAROL WAFORO

Elebor, Kaunti ya Marsabit

Baada ya malalamiko ya wakaazi wa eneo la Elebor kuhusu ukosefu wa maji safi, mamlaka ya maji jimboni Marsabit imeahidi kukarabati kisima hicho ifikapo mwishoni mwa juma hili.

Fakasa Boru Fakasa, Msimamizi wa Timu ya Kurekebisha Visima vya Maji, amebainisha kuwa awali changamoto ilikuwa kwenye pampu ya maji, ambayo ilisababisha ucheleweshaji wa ukarabati wa kisima hicho. Hata hivyo, Fakasa amekataa madai ya wakaazi kuwa kisima hicho kiliharibika miaka miwili iliyopita, akisema kuwa hicho kiliharibika mwezi Machi mwaka huu.

Kuhusiana na juhudi za ukarabati wa visima, Fakasa amesema kuwa mamlaka yanazidi kuendelea na kazi hizo katika maeneo mbalimbali ya kaunti, huku akitaja eneo bunge la Laisamis kama moja ya maeneo yanayofanyiwa kazi hiyo.

Changamoto za upatikanaji wa maji safi ni suala la msingi katika eneo la Marsabit, likichangiwa na ukame na uhaba wa miundombinu. Juhudi za mamlaka za maji za kukarabati na kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya maji ni hatua muhimu katika kukabiliana na changamoto hizo. Hii itasaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa maji safi kwa jamii za Marsabit.

Subscribe to eNewsletter