Local Bulletins

KNUT YATAKA WALIMU 44 WA JSS WALIOACHISHWA KAZI MARSABIT WAREJESHWE MARA MOJA

.

Na Samuel Kosgei

Muungano wa kitafa wa walimu KNUT tawi la Marsabit umeonesha wasiwasi wake kutokana na bajeti ya tume ya kuajiri walimu TSC kupunguzwa na serikali kwenye mabadiliko mapya yanayoshuhudiwa katika idara zote za serikali.

Katibu mkuu wa muungano huo wa KNUT tawi la Marsabit Rosemary Talaso Haro amesema kuwa kupunguzwa kwa bajeti hiyo bila shaka inamaanisha kuwa walimu elfu 46,000 waliokuwa waajiriwe na tume ya kuajiri walimu TSC kwa njia ya kudumu huenda isiwezekane ikiwa ni pamoja na kutopokezwa marupurupu na nyongeza ya mishahara kama walivyoelewana na serikali.

Sasa KNUT inaiomba serikali kurejesha mgao huo wa TSC ili kufanikisha mpango huo wa walimu wa JSS kuajiriwa kwa njia ya kudumu.

Wakati uo huo muungano huo unataka walimu 746 wa JSS waliotimuliwa kazini na tume ya TSC warejeshwe kazini kwani walimu hao huenda hawakufahamu athari za mgomo wao.

Kati ya walimu hao Zaidi ya mia saba, walimu 44 ni kutoka kaunti hii ya Marsabit.

Mwalimu Talaso pia ameitaka idara ya walimu hapa Marsabit kuwahusisha wanafunzi walemavu kwenye mashindano ya michezo ya wanafunzi wa JSS ambayo imefanyika Marsabit kuanzia siku ya Jumatatu.

Subscribe to eNewsletter