Marsabit yatajwa kuwa miongoni mwa kaunti zinazokuwa kwa kasi kimaendeleo.
January 15, 2025
Jamii zinazoishi katika eneo la Loiyangalani zimeshauriwa kuisha kwa Amani msimu huu wa krismasi.
Kauli hiyo imetolewa na katibu wa baraza la wazee la Turkana tawi la Loiyangalani, Mzee William Ebukut.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Mzee William amezitaka jamii zinazoishi katika eneo hilo kuasi kasumba ya kuibiana mifugo na badala yake wakumbatie Amani ambayo italeta maendeleo na ushirikiano katika eneo hilo.
Ebukut ameelezea kuwa ni wajibu wa kila mwanarika kuwa karibu na mifugo msimu huu wa sherehe ili kuboresha usalama wao.
Mzee Ebukut amesema kuwa ni sharti pia viongozi kuungana na kuacha kampeni za mapema kwa madhumuni ya kuleta Amani na maendeleo mashinani.
Katibu huyu ameshauri serekali pamoja na wahisani wanaosaidia katika kuandaa michuano za kandanda katika eneo la Loiyangalani kuweza kuhubiri Amani baina ya Vijana na jamii nzima ya eneo hilo.