Local Bulletins

IDARA YA USALAMA ENEOBUNGE LA LAISAMIS YALAUMIWA KWA KWA KUTOWACHUKULIA WANAOCHANGIA DHULMA ZA KIJINSIA

Na Carol Waforo

Idara ya usalama katika eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit imelaumiwa pakubwa kwa utepetevu na hivyo kuchangia ongezeko la Visa vya dhulma za kijinsia katika eneo hilo.

Hii ni kutokana na idadi ya juu ya madai vya visa vya ubakaji pamoja na ukeketaji wa mtoto msichana ambavyo vinarekodiwa huku washukiwa wakisalia kutowajbishwa kwa mujibu wa sheria.

Kulinga na afisa wa watoto eneo bunge Laisamis Umoro Diba visa vya dhulma za kijinsia vinaripotiwa katika vituo vya polisi ila washukiwa hawakamatwi.

Umuro ametoa mfano na kisa cha mtoto msichana wa miaka 16 aliyekeketwa kwa nia ya kuozwa hiyo jana katika eneo la Merille ambapo washukiwa wakuu hawajakamatwa hadi kufikia sasa na hata visa vya hapo awali ambapo washukiwa bado hawajawajibishwa.

Kulingana na Umuro afisi yake inarekodi visa kama vitano ya ubakaji kila mwezi.

Umuro pia amelaumu pakubwa wakaazi kwa kusuluhisha visa hivi kinyumbani badala ya kukumbatia hatua ya watuhumiwa kuwajibishwa kisheria.

Naye mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu Evanna Esekon ambaye ni mwasisi na mwenyekiti wa shirika la Loiyangalani Springs of Hope ametoa wito kwa waadhiriwa kufuata kesi zao hadi haki itakapopatikana.

Subscribe to eNewsletter