Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
NA CAROLINE WAFORO
Kulingana na afisa wa kufuatilia magonjwa ya mifugo jimboni Marsabit Dkt Bernard Chege ambaye amezungumza na shajara ni kuwa PPR ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoathiri haswa mbuzi na kondoo na umethibitishwa katika eneo pana la Chalbi ikiwemo Elbeso, Kalacha, Maikona, kati ya mengine.
Dr Chege anasema dalili za ugonjwa huo ni pamoja na vidonda kwenye mdomo, mbuzi kutokwa kamasi na machozi pamoja na ukosefu wa maji mwili jambo ambalo linasababisha hata vifo.
Aidha amedokeza kuwa ugonjwa huo sana hushuhudiwa katika kipindi cha ukame na kiangazi.
vilevile ameeleza kuwa ugonjwa huo huenda umeletwa na mifugo walionunuliwa kutoka nje ya jimbo hili kupitia fidia ya mifugo kwa wafugaji baada ya asilimia kubwa kufa kipindi cha kiangazi.
ugonjwa huo pia umeripotiwa nchini Ethiopia na huenda mifugo ya Kenya imetangamana mpakani.
Aidha Dr Chege amesema kuwa ugonjwa wa PPR hauna tiba japo kunazo dawa za kupunguza makali yake. Mfugaji ametakiwa kumpa mfugo aliyeadhirika maji mengi ikikumbukwa kuwa wanakufa kutokana na ukosefu wa maji mwilini.
Na haya yamejiri baada ya malalamishi kutoka kwa wafugaji wa eneo la Elbeso wadi ya Northhorr ambao wanadai kuwa takriban zaidi ya mbuzi 18 wamekufa kutokana na ugonjwa huo wa PPR.
Dr Chege amedokeza kuwa idara hiyo inafanya uchunguzi zaidi ili kubaini idadi ya vifo ambavyo vimeweza kushuhudiwa hadi kufikia sasa.
Wakati uo huo Idara hiyo imethibitisha kuzuka kwa ugonjwa wa haemorrhagic septicemia katika eneo bunge la laisamis kaunti ya Marsabit na unaathiri haswa ngamia.
Dr chege anasema kuwa ugonjwa huo unasababishwa na virusi vinavyoripotiwa kutokana na mabadilko ya hali ya anga.
kadhalika amedokeza kuwa a dalili zake ni ngamia kufura kichwa pamoja na joto mwilini.
Vilevile amethibitisha kuwa baadhi ya ngamia wameripotiwa kufariki dunia japo visa vyake ni vichache mno. Daktari chege anasema kuwa uchunguzi wao umebaini kuwa ugonjwa huo ni wa msimu.
Ugonjwa huo unathibitiwa kwa kuwatibu mifugo kutumia dawa japo dakatri chege anasema kuwa kunazo changamoto kwani wafugaji wanalazimika kuzinunua wenyewe kwa bei ghali.