photo courtesy
Local Bulletins

IDARA YA ELIMU KUSHIRIKIANA NA WASHIKADAU WENGINE, KUANGAZIA NAMNA SHULE YA MSINGI YA EL MOLO BAY INAWEZA HAMISHWA – CDE JOSEPH MAKI

NA ISAAC WAIHENYA

Idara ya elimu kaunti ya Marsabit itashirikiana na washikadau wengine, ikiwemo ofisi ya CDF katika eneo bunge la Laisamis na wizara ya usalama wa ndani kuangazia namna shule ya msingi ya El Molo Bay inaweza hamishwa katika eneo salama na mbali na maji ya ziwa Turkana katika siku za usoni.

Kulingana na mkurugenzi wa elimu kaunti ya Marsabit Joseph Maki ni kuwa hilo linatokana na kuongezeka kwa idadi ya maji ya ziwa Turkana kila kuchao jambo linalohatarisha maisha ya wanafunzi.

Maki aliyezungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani ofisini mwake ametaja kuwa japo hali kwa sasa sio mbaya vile, ila mikakati kabambe inafaa kuwekwa ili kuhakikisha kwamba wanafunzi shuleni humo wako salama.

Shule ya msingi ya El Molo Bay ni baadhi ya taasisi ambazo zimeadhirika kutokana na kuogezeka maradufu kwa maji ya ziwa Turkana ambayo pia yameadhiri barabara kadhaa na hata kanisa Katoliki eneo hilo.

Subscribe to eNewsletter