Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Grace Gumato
Msimamizi wa idara ya chanjo ya watoto katika kaunti ya Marsabit Abdub Boru amesema kuwa Idadi ya watoto wanaopokea chanjo katika kaunti ya Marsabit imepungua kutoka mwaka wa 2021.
Boru amesema kuwa kaunti ndogo ya North Horr ndiyo iko na idadi ndogo ya watoto ambao wameweza kupata chanjo na hiyo anasema imechangiwa na jamii kutoka sehemu hiyo kuwa wafugaji wa kuhamahama.
Aidha Boru amesema kuwa kulikuwa na upungufu wa chanjo tatu ambao ni BCG, Measles (Rubella Vaccine) na chanjo ya kupitia mdomoni kwa muda wa wiki mbili lakini kwa sasa serikali imeweza kupata chanjo hizo.
Hata hivyo Boru amehimiza jamii kuwapeleka watoto waweze kupata chanjo ili kuepukana na magonjwa kama vile kifua kikuu na Rusua(measles).