Marsabit yatajwa kuwa miongoni mwa kaunti zinazokuwa kwa kasi kimaendeleo.
January 15, 2025
Wizara ya afya kaunti ya Marsabit imezindua Ambulensi 4 katika juhudi za kuboresha utoaji wa huduma za afya jimboni.
Uzinduzi wa ambulensi hizo na ambazo ni ukarabati wa ambulansi zilizokuwa zimetumika hapo awali ulifanyika hapo siku ya Jumatatu.
Akizungumza na shajara ya radio Jangwani afisini mwake waziri wa afya jimboni Marsabit Malicha Boru amesema kuwa ambulansi hizo nne zilifadhiliwa na shirika la Medecins Du Monde na kugharimu shilingi milioni 2.3
Kulingana na waziri Malicha ambulansi hizo tayari zimeanza kutumika ambapo anasema kuwa zinatarajiwa kupiga jeki huduma za matibabu katika maeneo bunge yote manne jimboni.
Waziri amesema kuwa, kando na ambulansi hizo nne, serikali ya kaunti ya Marsabit ikiongozwa na gavana Mohamud Ali itazindua ambulansi nyingine mpya ikiwemo nne zilizonunuliwa na serikali ya kaunti ya Marsabit kwa kima cha shilingi milioni 50.
Uzinduzi huo utafanyika katika eneo bunge la Moyale wakati wa kambi ya matibabu ya bure MEDICAL Camp inayotarajiwa kufanyika katika hospitali ya rufaa ya Moyale kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 21 December.
Kambi hiyo ya matibabu itathaminiwa na shirika la Muslim University Association kwa ushirikiano na hospitali kuu ya Kenyatta pamoja na hospitali ya rufaa ya Marsabit na inatarajiwa kutoa huduma wakaazi kutoka kote jimboni.
Wakati uo huo Wakaazi wametakiwa kuchukua fursa hii kujisajili ili kupokea matibabu hayo ya bure shughuli itakayoongozwa wataalam mbalimbali wa afya.