Local Bulletins

IDADI YA VISA VYA DHULMA ZA KIJINSIA YAONGEZEKA JIMBONI MARSABIT. – ASEMA MWANAHARAKATI NURIA GOLLO

NA GRACE GUMATO

Visa vya dhulma za kijinsia yameripotiwa kuongezeka maradufu jimboni Marsabit idadi hiyo ikitajwa kuongezeka kutokana na mabailiko ya tabia nchi na umaskini miongono mwa jamii za wafugaji.

Akizungumza na idhaa hii ofisini Mwake Nuria Gollo ambaye ni mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu amesema kuwa wanaoadhirika pakubwa na dhulma hizi ni akinamama.

Nuria amekariri kuwa hali ya kiangazi iliyoshuhudiwa mwaka jana hapa jimboni Marsabit imesababisha kuongezeka kwa matukio ya dhulma za kijinsia manyumbani kwani wanandoa wengi hawana uwezo wa kuzikimu familia zao.

Aidha Nuria amesema kuwa dhulma za kinjisia zimesababisha akimama kuachiwa majukumu ya kulea watoto wakiwa pekee yao hali ambayo imechangia watoto wengi kuacha shule kwa ajili ya ukosefu wa karo.

Hata hivyo Nuria amewashauri akinamama wanaodhulumiwa kutonyamazia visa hivyo na kuwarai kuripoti katika idara husika ili kupata usaidizi.

Subscribe to eNewsletter