Local Bulletins

HUDUMA ZA MAJI MJINI MARSABIT KUREJELEWA MWISHONI MWA WIKI HII HUKU ZOEZI LA KUSAFISHA BWAWA LA BAKULI 2 LILIKARIBIA TAMATI.

Na Samuel Kosgei

ZOEZI la kutoa mchanga na kuondoa uchafu kutoka bwawa la Bakuli 2 ulio mlima Marsabit linakaribia kukamilika huku asilimia zaidi ya 90 ikiwa imefanyika kufikia sasa.

Hayo ni kulingana na meneja msimamizi wa kampuni ya maji na majitaka kaunti ya Marsabit MARWASCO Stephen Sora Katelo alipozungumza na wanahabari baada ya kutembelea eneo hilo kutathmini kazi inayoendelea.

Katelo amezidi kuomba wananchi wa mji wa Marsabit kuwapa muda kiasi huku akiahidi shughuli za usambazaji wa maji mjini Marsabit kurejelewa mwishoni mwa wiki hii au mwanzo wa wiki ijayo.

Mwakilishi wadi wa Marsabit Central Jack Elisha ambaye wadi yake imeathirika zaidi na ukosefu wa maji amesisitiza haja ya wananchi kuipa muda kiasi kampuni hiyo kukamilisha kuondoa uchafu kwenye bwawa hilo muhimu kwani zoezi hilo lilifanyika mwisho mwaka wa 1997.

Kauli yake pia imekaririwa na chifu wa lokesheni ya Jirime Enock Kallo ambaye amesema mageuzi yanayofanywa na MARWASCO yatawafaa watumiaji maji hayo zaidi.

Subscribe to eNewsletter