Local Bulletins

HOFU YA UHABA WA CHAKULA KATIKA KAUNTI YA MARSABIT BAADA YA WAKULIMA KUKADIRIA HASARA WAKATI WA MVUA FUPI YA MWEZI APRILI

Na JB Nateleng,

Huenda kukashuhudiwa uhaba wa chakula katika kaunti ya Marsabit baada ya wakulima wengi kukadiria hasara ya mavuno wakati wa mvua fupi ya mwezi Aprili.

Kulingana na Dub Nura ambaye ni Afisa wa kilimo katika kaunti ndogo ya Saku ni kuwa mavuno ya msimu huu hayawezi yakakimu mahitaji ya wakaazi wa Marsabit na kuongezea kuwa vyakula vinavyotoka katika taifa jirani la Ethiopia na kaunti zingine humu nchini ndivyo viko sokoni na kuleta bei mpya ambayo huenda pia ikaathiri biashara nyingi jimboni.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipee Dub amesema kuwa chakula kilichoko huenda kikasaidia kwa kipindi cha muda wa mwezi moja na nusu pekee.

Afisa huyu wa kilimo amewataka wakulima kufuata mawaidha kutoka kwa idara ya utabiri wa hali ya hewa kujua ni muda upi wanapaswa kupanda na kupalilia ili waepukana na hasara kama ilivyokuwa hapo awali.

Hata hivyo Dub amepongeza hatua ya wakulima ya kuamua kujitegemea badala ya kuongojea msaada ambao mara nyinyi huchelewa akisema kuwa hatua hiyo itasaidia katika kukuza na kuimarisha kilimo jimboni.

Ameelezea kuwa kufikia sasa wakulima wamejipanga vilivyo na huenda kukawa na mavuno mengi mwaka ujao iwapo msimu wa mvua hautabadilika.

Subscribe to eNewsletter