Local Bulletins

HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.

UKOSEFU wa elimu ya kutosha kuhusu bima ya afya ya SHA ndio sababu kuu ya watu kutojisajili  katika kaunti ya Marsabit. Haya ni kwa mujibu wa meneja wa mamlaka ya SHA katika kaunti ya Marsabit, Kaaria Mutuma.

Akizungumza na idhaa hii afisini mwake, Mutuma ameelezea sababu kuu zinazoathiri kusajili kwa bima hiyo  ya afya kwa wakaazi wa jimbo hili ikiwemo  ukosefu wa rasilimali za  kuwafikia wakaazi wengi wanaoishi katika maeneo ya mbali.

Aidha, Mutuma amedokeza kuwa hospitali za kibinafsi katika kaunti ya Marsabit  bado zinakataa kuandikisha kandarasi ya bima hiyo japo afisi yake inaendelea na juhudi za kuwahusisha ili waweze kujisajili na kusaini kandarasi.

Ameongeza kwamba, hospitali ya serikali zimetia sani kandarasi hizo na inawahudumia wagonjwa bila tatizo lolote.

Subscribe to eNewsletter