Local Bulletins

GAVANA WA MARSABIT AWATAKA MAAFISA WA USALAMA WANAOLINDA MIGODI YA DHAHABU DABEL KUONDOLEWA.

Gavana wa Marsabit Mohamud Ali sasa anawataka maafisa wote wa usalama wanaolinda migodi ya dhahabu ya Hillo kule Dabel eneo bunge la Moyale kuondolewa mara moja.

Gavana Ali amedai kuwa maafisa hao wanajinufaisha na biashara ya dhahabu licha ya serikali kutangaza kufungwa kwa migodi hiyo.

Gavana Ali akizungumza kwenye maadhimisho ya jamhuri dei amesema kuwa maafisa wa usalama Marsabit walimpotosha inspekta wa polisi kwa kutosema ukweli kuhusu vifo vya Dabel, suala analosema kuwa italeta picha mbaya kwa utawala wa sasa.

Wachimba migodi kadhaa wanadaiwa kufa siku Jumanne katika migodi hiyo baada ya kuzikwa na mchanga.

Hata hivyo Inspekta jenerali wa Polisi Douglas Kanja Jumatano alikana kuwa hakuna maafa yoyote yaliyotokea katika eneo hilo.

Wakati huo Gavana Ali amemtakata mwenzake wa Isiolo Ibrahim Guyo kukoma kuingilioa maswala yanayohusu jimbo hili.

Gavana wa Isiolo anadaiwa kuchochea jamii moja eneo hilo la Dabel kuwa ardhi yao inanyakuliwa.

Kiongozi wa jimbo amewataka wakazi wa jimbo hili kujisajili kwa wingi katika mfumo mpya wa Afya wa SHA akisema unamanufaa makubwa.

Subscribe to eNewsletter