Local Bulletins

Familia elfu 4 Marsabit kufaidika na mpango mpya wa NDMA ambao watapewa nyongeza ya sh.1000 kudhibiti utapiamlo.

Na Samuel Kosgei

Mamlaka ya Kitaifa ya Kudhibiti Ukame na majanga (NDMA) tawi la Marsabit, kwa sasa inaendeleza zoezi la kusajili familia 4000 ambazo zinapaswa kupokea Ksh.3,700 kila mwezi katika mpango mpya wa kukabiliana na njaa HSNP.

Mratibu wa mamlaka hiyo hapa Marsabit Guyo Golicha Iyya alisema kuwa Familia hizo zimekuwa zikipokea Sh.2,700 kila mwezi na kuanzia mwezi ujao watapata Sh.1000 zaidi ili kudhibiti Utapiamlo kwa watoto walio chini ya miaka 5 katika maeneo bunge manne ya Marsabit ambazo ni pamoja na: Laisamis – 1059, Moyale – 1095, North Horr – 866 + (Illeret 92) na Saku 888

Golicha akizungumza na kituo ofisini mwake alisema kuwa lengo la serikali ni kusaidia wakaazi wa Marsabit maliza tatizo la utapiamlo ambalo kwa muda limekuwa kero kwa familia nyingi haswa katika maeneo kame.

“Sasa tunaomba wananchi watembelee ofisi za machifu ili wafahamu kama majina yao yapo kwenye orodha ya watu wanaofaa kufaidi kwenye mpango huo” Golicha alisema.

 

Golicha idhaa aliongeza kuwa kero la Utapiamlo lipo sana jimbo hili na hivyo kusema serikali iliona kuna haja wazazi kuwapa lishe bora watoto wao ili kupunguza ongezeko la ugonjwa huo.

Subscribe to eNewsletter