Local Bulletins

ELIMU DUNI YATAJWA KAMA CHANZO KIKUU KWA WASICHANA KUPATA MIMBA ZA MAPEMA JIMBO LA MARSABIT

Huenda ukosefu wa elimu yakutosha kwa wasichana kikawa chanzo kuu ya wasichana kupata mimba katika kaunti ya Marsabit.

Haya ni kwa mjibu wa mashauri katika mradi ya Gaddis Gamme Halima Ibrahim Golicha, mpango ambao hulenga kuelimisha kufunza wasichana namna ya kutetea haki zao na kujilinda kutokana na mathara ya jamii.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani wakati wa mafunzo ya wasichana katika shule ya upili ya Moi girls,Halima amesema akinamama ndio pekee hupokezwa elimu ya uzazi wakati wanapozuru kliniki huku wasichana nao wakisahaulika.

Halima ametaja athari za mimba za mapema kwa wasichana  ikiwemo kuacha shule pindi wanapotungwa mimba  jambo ambalo inawafanya wakose kutimiza ndoto yao maishani.

Hata hivyo Halima amewapongeza wazazi wanaowatunza wanao kwa njia nzuri huku akiwataka wazazi kuwa karibu na wanao ili wajue changamoto wanaopitia watoto haswa wasichana.

Adha mshauri huyo amewahimiza wasichana kutofuata  shinikizo la ujana na badala yake kuwasikiza wazazi wao kando na masuala ya ukeketaji na ndoa za mapema

Subscribe to eNewsletter