Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Na JB Nateleng
Dhulma za kijinsia na maswala ya unyanyapaa yametajwa kuwa sababu kuu inapelekea watoto wengi katika kaunti ya Marsabit kuweza kuadhirika kiakili.
Kulingana na Victor Karani ambaye ni afisa anayeshughulikia maswala ya afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Marsabit ni kuwa watoto wengi jimboni wanakataa kuripoti visa vya dhulma za kijinsia wakihofia maisha yao.
Amewataka wazazi kuwa karibu na wanao ili kuweza kuwasaidia kupambana na dhulma hizi ambazo zingine zinatokana na mtindo wa familia.
Mtaalam huyu wa afya ya akili amedokeza kuwa ni sharti wazazi waweze kuwalea wanao katika mazingira safi yasiyokuwa na kasoro yeyote kwani watoto wengi huadhiriwa na namna ya malezi.
Aidha Karani amesikitikia idadi ndogo ya watu wanaotembelea kliniki ya afya ya akili jimboni huku akiitaka serekali kuwekeza zaidi katika idara ya afya ya akili ili kuwawezesha wataalm wa kitengo hicho kuwatembelea wananchi na kutoa huduma kwao.