HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Samuel Kosgei
KAMATI ya fedha na mipango katika bunge la kaunti ya Marsabit imeitaka wananchi wa Marsabit kuhudhuria na vikao vya kudhibitisha miradi waliopendekeza kwenye mikutano ya hapo awali.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya fedha Daud Tomasot akizungumza na kituo amesema kuwa ni vyema wananchi kuhudhuria vikao hivyo ili kudhibitisha kuwa miradi waliopendekeza imenakiliwa na idara mbalimbali za serikali.
Anasema kuwa mara wakati mwingine miradi waliopendekeza huenda ikatolewa na nyingine kuongezwa bila ufahamu wa wananchi hivyo ni vyema kudhuria vikao vya kutoa maoni ili kudhibitisha miradi waliopendekeza.
Amedhibitishia kituo hiki kuwa bajeti iliyopendekezwa na wizara ya fedha ni takribani shilingi bilioni 9.1bn katika mwaka wa kifedha 2024/25.
Kulingana na ripoti hiyo ya makadirio ya bajeti, wizara ya huduma za afya ndio iliyotengewa mgao mkubwa wa fedha ambao ni takribani shilingi bilioni 2.05bn ikifuatwa na wizara ya kilimo, ufugaji na uvuvi iliyotengewa bilioni sh.1.1bn.
Idara iliyotengewa mgao mdogo wa fedha kwa bajeti hii ni ofisi ya katibu wa kaunti iliyotengewa shilingi milioni 11.
Tomasot ambaye pia ni MCA wa wadi ya Korr/Ngurnit ameitaka serikali ya kaunti kutia juhudi katika kukusanya ushuru wake wa ndani kwani mara nyingi haijakuwa ikitimiza lengo lake la kukusanya ushuru kama ilivyopanga.
Katika mwaka wa kifedha uliopita wizara ya fedha haikuweza kufikisha milioni 190 walikuwa wakilenga kukusanya kutoka kwa shughuli zake.
Mwaka huu kifedha wa 2024/25 wizara imejiwekea shabaha ya shilingi milioni 110 kufikia mwisho wa mwaaka wa kifedha ujao.
Changamoto kuu inasalia kudhibiti matumizi ya pesa za umma kwani kati ya shilingi 9bn, asilimia 36 inatumika kufanya maendeleo huku asilimia 64 ikiendea matumizi ya kila mwezi ikiwemo mishahara ya wafanyakazi.