Local Bulletins

Afueni kwa shule ya Loglogo Girls baada ya kujengewa nyumba ya walimu  na shirika KDEF

NA GRACE GUMATO

Ni afueni kwa shule ya bweni ya wasichana ya Loglog girls baada ya shirika lisilo la kiserikali la KDEF kujenge nyumba ya walimu  iliyofunguliwa rasmi hii leo katika shule hiyo.

Akizungumza katika halfa hiyo Ahmed Kura ambaye ni mkurungezi wa KDEF ni kuwa Zaidi ya shule 100 katika eneo bunge la Laisamis  zimeweza kujengewa nyumba ya walimu huku akitaja kuwa  walimu ni watu muhimu katika jamii kutokana na jukumu lao la kupiga jeki swala la elimu.

Hata hivyo amesema kuwa changamoto ni kwa wazazi ambao hawadhamini masomo akiwashauri wazazi kupeleka watoto shule za karibu kutokana  na gharama ya chini.

Aidha  Ambrose Harugura ambaye ni mkurungenzi wa bodi ya kuajiri wafanyakazi wa kaunti amesema kuwa kwa miaka ya nyuma jamii za wafugaji zimekuwa nyuma sana kwa maswala ya elimu huku akishukuru shirika la KDEF  kwa kuwasaidia jamii za wafugaji katika  kupiga jeki swala la elimu.

Mwalimu mkuu wa shule ya Logologo Rose Sagaram amerudishia  shirika la KDEF shukrani kwa kujengea nyumba walimu wake sawa na ofisi muhimu

Hata hivyo Alio Abdulahi ambaye ni mkurugenzi wa elimu katika kaunti ndogo ya Laisamis amesema kupitia shirika hilo watoto wengi wameweza kurudi shule na kulipiwa karo hivyo amewahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao shule akitaja jamii za wafugaji kuwa na hulka ya kupeleka watoto wao kuchunga mifugo.

Subscribe to eNewsletter