Idara ya misitu KFS Marsabit yaweka mikakati kuzuia moto kutoka Isiolo kufika Kaunti ya Marsabit
January 23, 2025
Chama cha ODM tawi la Marsabit jana kiliandaa chaguzi zake za mashinani huku wawakili mbalimbali katika vituo vya kupigia kura wakichanguliwa.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya chama hicho katika kaunti ya Marsabit Stephen Basele ni kuwa ni wanachama wa chama hicho 3,125 ambao waliruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi wa hapo jana.
Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, Basele amesema kuwa uchaguzi huo ulilenga kuwapata watakao wakilisha vituo mbalimbali vya kupigia kura ambao mapema mwaka ujao wa 2025 watawachagua viongozi wa kaunti pamoja na viongozi wa kitaifa.
Aidha Basele ameleza kwamba uchaguzi huo uliendelea kama ulivyoratibiwa katika maeneo mbalimbali hapa jimbo huku maeneo yaliyoadhirika na mvua yakiwasilisha matokeo yake hii leo asubuhi.