Local Bulletins

WAKAAZI WA MARSABIT WATOA HISIA ZAO KUHUSIANA NA MAADAMANO YA VIJANA WA GEN ZS (NANENANE)

Na Ebinet Apiyo,

Baadhi ya wakaazi mjini Marsabit wamewataka vijana wa Gen Zs kusitisha maadamano yao yaliyopangwa kufanyika hapo kesho na badala yake kumpa rais muda wa kufanya kazi haswa baada ya kutekeleza mageuzi kadhaa serekali.

Baadhi ya waliozungumza idhaa hii wameyataja maadamao ya hapo kesho yaliyopewa jina NANENANE kama yanayolenga tu kuhujumu utendakazi wa serekali.

Wengine wao wamelalamikia kuadhirika kwa biashara haswa wakati wa maadamano kwani biashara nyingi huishia kufungwa kwa hofu ya kuzuia uharibu kutoka kwa waadamanaji.

Hata hivyo baadhi yao wameunga mkono maandamano ya kesho wakidai kwamba ndio njia pekee ya kumfanya Rais kuskiza matakwa yao.

Subscribe to eNewsletter