Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
NA SAMUEL KOSGEI
Walimu wa shule za chekechea katika kaunti ya Marsabit wamepokezwa mafunzo ya kidijitali hatua ambayo inalenga kuwafaa wanafunzi 11 katika kaunti ndogo zote za Marsabit.
Afisa mkuu katika idara ya elimu kaunti ya Marsabit Qabale Adhi alisema kuwa walimu wote wa ECDE watapokea mafunzo hayo ya kusomesha watoto kwa njia ya kidigitali kwani silabasi yote ya chekechea imehifadhiwa katika vifaa vya kisasa.
Anasema kuwa kwa sasa machine hizo zina silabasi na mafunzo ya masomo ya Kiingereza na Kiswahili kwa wanafaunzi huku masomo yote pia yakitarajiwa kuwekwa kwenye mashine hizo.
Qabale alisisitiza kuwa mafunzo hayo sana yanaegemea suala la umilisi ambapo wanafunzi wataona na kufanya mafunzo kinyume na sasa ambapo wanafunzwa masuala ya kufikirika tu.
“Kila kituo cha ECDE kitapata vifaa viwili vya masomo ya digitali itakayotumika na madarasa ya pp1 na pp2. Alisema Qabale.
Walimu wa shule za chekechea Marsabit ni Zaidi ya 490 wote walio kwenye kandarasi na hata wale wa kudumu.