Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
NA SAMUEL KOSGEI
Katika juhudi za kukuza kilimo miongoni mwa vijana, wazazi katika Kaunti ya Isiolo wameombwa kuwashirikisha watoto wao katika shughuli za ukulima, kuanzia kiwango cha vijiji na katika wadi mbalimbali.
Wito huu umetolewa na Charlene Ruto, binti ya Rais William Ruto, wakati alipofanya ziara katika Kaunti ya Isiolo ili kutembelea akina mama wanaojihusisha na kilimo-biashara katika wadi ya Ngaremara. Charlene amepongeza juhudi za akina mama hao na kuwahamasisha zaidi kujihusisha na ukulima na ufugaji wa nyuki.
Akina mama wakulima katika wadi ya Ngaremara walikuwa tayari wamepokea mafunzo na msaada kutoka kwa shirika la World Vision kwa ushirikiano na KOICA, jambo lililowapa nguvu ya kuanza na kuendeleza shughuli zao za kilimo-biashara.
Jitihada hii kutoka Kaunti ya Isiolo inaendana na juhudi zaidi nchini za kukuza ushiriki wa vijana katika kilimo, sekta ambayo bado ni muhimu kwa usalama wa chakula na maendeleo ya kiuchumi ya nchi. Kwa kuwashirikisha watoto mapema, kaunti inategemea kulea kizazi cha wakulima na wafanyabiashara wa kilimo watakaobadili mandhari ya kilimo miaka ijayo.