Local Bulletins

Na Caroline Waforo

Serikali itatumia shilingi milioni 612 ili kuunganisha kaunti ya Marsabit na mfumo wa umeme wa taifa, National grid kutoka Loiyangalani hadi mjini Marsabit.

Haya yamebainika katika uzinduzi wa nne wa mpango wastani ambao unajumuisha kipindi cha mwaka 2023-2027, kikao cha kuhusisha umma na ufafanuzi wa programu ya maendeleo katika kaunti ya Marsabit, hafla iliyoandaliwa katika ukumbi wa kanisa katoliki.

Fedha hizo Milioni 612 zimejumuishwa katika bajeti inayotarajiwa kusomwa wiki hii na waziri wa fedha. Njuguna Ndungu.

Kadhalika serikali itatumia bilioni 1.5 kuunganisha umeme kutoka kaunti ya Marsabit hadi katika kaunti ya Isiolo.

Kello Harsama ni katibu katika wizara ya maeneo kame.

Subscribe to eNewsletter