Local Bulletins

WAUZAJI WA MUGUKA NA MIRAA MARSABIT WANAONEWA DHIDI YA MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI

NA CAROLINE WAFORO

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mazingira Taifa (NEMA), Naftaly Osoro, amewaasa vikali wauzaji wa muguka na miraa katika Kaunti ya Marsabit dhidi ya matumizi ya mifuko ya plastiki, ambayo imepigwa marufuku tangu mwaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu, Osoro amesema kuwa NEMA inashirikiana na idara ya usalama pamoja na serikali ya kaunti ya Marsabit ili kuhakikisha marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki inatekelezwa kikamilifu.

Aidha, Osoro amebainisha kuwa karatasi za plastiki zimekuwa zikitumika sana katika Kaunti ya Marsabit, licha ya marufuku hiyo iliyowekwa na serikali chini ya utawala wa rais mstaafu Uhuru Kenyatta mwaka 2017. Kumekuwa na madai kwamba mifuko hii huingizwa nchini kwa njia ya magendo kuelekea katika mpaka kati ya Kenya na Ethiopia.

Kwa hivyo, NEMA imetoa onyo kali kwa wauzaji wa muguka na miraa katika Marsabit dhidi ya matumizi ya mifuko ya plastiki, ikishirikiana na vyombo vya usalama na serikali ya kaunti ili kuhakikisha marufuku hii inatekelezwa.

Subscribe to eNewsletter