Local Bulletins

Wazazi Marsabit Wahimizwa Kuwalinda Watoto Dhidi ya Mitandao ya Kijamii

Na Grace Gumato

Wazazi na walezi kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwaongoza vyema watoto wao katika matumizi sahihi na salama ya mitandao kwani wengine wao hujifunza tabia za kuwapotosha kimaadili kupitia mitandao.

Wito huu ulitolewa na Thomas Mugo ambaye ni Afisa wa Masuala ya Watoto kaunti ya Marsabit kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto Muafrika katika  shule ya wasichana ya St. Teresa mjini Marsabit.

Mugo alisema kuwa serikali itaendelea kuhamasisha matumizi bora ya mitandao ili kuwaepusha watoto na masuala yasiyo na madhili mema katika jamii.

Aidha Mugo alitoa wito kwa wazazi na walezi kukuza talanta za watoto wao vile vile kuwasaidia kuimarisha talanta hizo.

Nuria Gollo ambaye ni mtetezi wa haki za kibinadamu kaunti ya Marsabit alisema kwamba watoto wanahitaji wosia wa wazazi na kwamba pia ni muhimu mzazi  kumsikiliza mtoto wake.

Siku ya Kimataifa ya Mtoto Muafrika huadhimishwa Juni 16 kila mwaka tangu mwaka 1991 kwa lengo la kuhamasisha jamii kujadili, kutathmini na kuweka mikakati ya kuboresha maisha ya mtoto wa kiafrika kama msingi wa kujenga taifa bora.

Siku hii ilianzishwa na Jumuiya ya Umoja wa Afrika (OAU) na kuadhimishwa kwa mara ya kwanza Juni 16, 1991 ili kuwahimiza viongozi kujenga utashi wa kisiasa wa kushughulikia matatizo yanayowakabili watoto wa Kiafrika kwa kuweka sheria za kuwalinda pamoja na kuwajengea mazingira bora ya kuishi.

“Kauli mbiu ya mwaka huu inasisitiza kuzingatia usalama wa mtoto katika ulimwengu wa kidigitali.

Subscribe to eNewsletter