Local Bulletins

Wakaazi wa Kaunti ya Marsabit Wahimizwa Kujitokeza kwa Wingi Kutoa Damu ili Kuokoa Maisha

Afisa Mkuu Mtenday wa MCRH Kussu Abduba akizungumza katika kituo cha kutoa damu kwenye hospitali ya rufaa ya Marsabit, Jumatano 14, 2023

Na Isaac Waihenya

Huku ulimwengu ukiadhimidha siku ya kutoa damu duniani wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kutoa damu.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu Mtendaji katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Kussu Abduba ni kuwa kutoa damu kuna faida sio tu kwa wanaohitaji damu mbali pia kwa anayetoa damu.

Akizungumza na Radio Jangwani katika kituo cha kutoa damu kwenye hospitali ya rufaa ya Marsabit Kussu alisema kuwa hitaji la damu hapa jimboni huongezeka kila kukicha kutokana na ongezeko la idadi ya watu pia huku akiwarai wakazi wa Marsabit kutosikiliza dhana potovu kuhusu utoaji wa damu.

Mwanahabari wa Radio Jangwani James Wanyonyi akitoa damu katika hospitali ya MCRH, Jumatano 14 Juni 2023

Wito sawia na huo ulitolewa na aliyekuwa mwaniaji wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Saku kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwa tiketi ya chama cha ANC Mamo Waqo Mado ambaye alisisitiza hoja ya kutoa damu mara kwa mara na pia wakati kuna hitaji la damu ili kuokoa Maisha.

Aidhaa Baadhi ya waliofika kutoa damu pia walilezea umuhimu wa kufanya vile na kwamba hakuna madhara yeyote kwa anayetoa damu.

Vilevile baadhi ya wafanyikazi wa Radio Jangwani wakiongozwa na Meneja Denson Machuki pia walihusika katika zoezi hilo na kutoa hamasa kwa wananchi wa Marsabit pia kukumbatia zoezi hilo ili kuokoa maisha.

 

 

Subscribe to eNewsletter