WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na John Bosco Nateleng
Visa vya mimba za mapema kwa watoto wasichana vinazidi kuripotiwa katika kaunti ya Marsabit. Haya ni kwa mujibu wa Mtetezi wa haki za kibinadamu jimboni Nuria Gollo.
Akizungumza na wanahabari hapa mjini, Nuria alitaja kwamba eneo bunge la Saku ndio imeripoti visa vingi vya mimba za mapema huku eneo bunge la North horr ikiripoti visa vingi vya ndoa za mapema.
Pia Gollo alitaja kwamba swala la ukosefu wa usalama umechangia pakubwa katika kuathiri masomo ya wanafunzi. Alitaja kuwa watoto wengi wanatembea masafa marefu kupata elimu hivyo kuhatarisha maisha yao.
Aidha Gollo alisema kuwa wasichana wengi katika kaunti ya Marsabit wanapitia changamoto si haba haswa ukosefu wa vitambaa vya sodo, hivo kuwafanya kusalia nyumbani wakati wenzao wanaendelea na masomo.
Hata hivyo Gollo aliwarai wazazi na walezi kuwapeleka watoto shuleni na kutokomeza ndoa za mapema na ukeketaji wa wasichana.