Local Bulletins

Viongozi wa Saku Youth Assembly Wakula Kiapo Rasmi Kuanza Majukumu

Wanachama wa Bunge la Vijana, Saku Juni, 21 2023

Na Isaac Waihenya

Viongozi wa Bunge la Vijana katika eneo Bunge la Saku maarufu kama Saku Youth Assembly wamekula kiapo cha kuanza kazi rasmi , zoezi ambalo liliandaliwa katika mkahawa wa Jirime hapa mjini Marsabit.

Akizungumza baada ya zoezi hilo mratibu wa mipango katika shirika la Mabadiliko endelevu (IFPC) Hassan Mulata alitaja kwamba uwepo wa bunge hilo utasaidia vijana katika kuwasilisha hoja zao kwa viongozi husika sawa na kuhakikisha kwamba maoni ya vijana mashinani yanafikia wahusika.

Mulata alisema kuwa bunge hilo lenye   wanachama 22 litakuwa na kamati za bunge tatu huku likitarajiwa kuchagua spika wake hivi karibuni.

Aidha mkurugezi katika idara ya vijana kauti ya Marsabit ambaye pia alifika katika hafla hiyo Jillo Ibrahim, aliwataka vijana hao kuwa mfano mwema unaoweza kuigwa na vijana wengine jimboni na pia kuwa mabalozi wa Amani.

Baadhi ya vijana waliozungumza baada ya Kula kiapo wakiongozwa na Abulaziz Boru walisema kuwa watatumua muugano huo kusukuma ajenda za vijana katika eneo Bunge la Saku na kaunti nzima kwa ujumla.

Walitaja kwamba mengi ya maswala ya vijana katika kaunti ya Marsabit yalikuwa yakipuuzwa ila kwa sasa watatumia umoja wao kuhakikisha kwamba maswala ya hayo yanapewa kipau mbele.

Subscribe to eNewsletter