HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
Na Samuel Kosgei
Mwakilishi wa kike kaunti ya Marsabit Naomi Jilo Waqo amekariri haja ya wananchi wa Marsabit kuzidi kuishi kwa amani na kuzidi kuvumiliana kwa minajili ya maendeleo ya jimbo.
Akizungumza na kituo hiki kwenye kipindi cha Bunge Letu Asubuhi, Naomi alikumbusha umuhimu wa kuishi kwa uwiano kati ya jamii hasimu. Alisema kuwa yeye pia yuko radhi kufanya maridhiano na wapinzani wake kwa njia ya heshima kwani ni kupitia ujio wa pamoja ndipo viongozi wanaweza kuzungumza kwa sauti moja.
Aidha alisema kuwa serikali kuu imeweka mikakati mwafaka kuweza kuanzisha miradi ya maji katika jimbo hili haswa kuanzishwa upya kwa bwawa la Badasa na uchimbaji wa mabwawa mengine ili kuwezesha kilimo cha unyunyizaji na maji ya mifugo.