KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Silvio Nang’ori
Maonyesho ya kwanza ya biashara kaunti ya Marsabit yamefunguliwa rasmi hapa mjini Marsabit.
Wafanyibiashara mbalimbali na mashirika ya serikali na yale yasiyo ya kiserikali walijumuika katika uwanja wa Marsabit kuonyesha bidhaa na huduma zao kwa umma.
Wakizungumza na idhaa hii baadhi ya washiriki walielezea matumaini kwamba maonyesho hayo ya siku tatu yatasaidia pakubwa katika kuimarisha biashara na uwekezaji kwa faida ya kaunti.
Wafanyibiashara hao hasa waliiomba serikali ya kaunti na ile ya kitaifa kuwasaidia kupata mikopo ili kusaidia baishara zao kuimarika.
Kwa upande wake waziri wa Biashara na ushirika kaunti ya Marsabit Adan Hirbo Oche alitaja kufurahishwa na idadi kubwa ya washiriki waliojitokeza leo hii akisema ni dhihirisho kwamba kaunti hii ina uwezo wa kuzalisha bidhaa vile vile kuvutia wawekezaji.
Aliwataka wafanya biashara na wawekezaji kuweka juhudi na jitihada zaidi katika biashara yao na kushiriki kwa pamoja katika kuleta maendeleo ya kaunti.