Local Bulletins

Mama amkatakata mwanawe na kula maini yake huko Kitengela kaunti ya Kajiado.

Picha; Hisani

Na Isaac Waihenya,

Polisi mjini Kitengela kaunti ya Kajiado wanamzuilia mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 27 ambaye anadaiwa kumua mwanawe mwenye umri wa maiaka 2 kwa kumkata kata vipande kwa kisu, kisha akala sehemu za ndani za mwili wa mtoto huyo kama vile maini na matumbo.

Kamanda wa Polisi kwenye kaunti ndogo ya Isinya Patrick Manyasi amethibitisha kisa hicho, akisema mwanamke huyo ambaye alikuwa amerejea kwa wazazi wake katika mtaa wa milimani, kutoka nyumbani kwake huko Kirinyaga, alijifungia nyumbani kwa wazazi wake na kumtendea mtoto huyo unyama huo.

Manyasi anasema kamsa kutoka kwa mtoto huyo ndio iliwaavutia majirani ambao walifika nyumbani humo na kukutana na tukio hilo la kushangaza, ambapo mtoto huyo alikuwa amekatwa katwa vipande na sehemu kadhaa kuliwa na mama huyo ambaye baadae alipoteza fahamu.

Kwa sasa mwanamke huyo ambaye alipelekewa hospitalini na kutibiwa anazuliwa katika cha Polisi cha Kitengela,huku polisi wakiendelea kupekua ushahidi zaidi kabla ya kumfikisha kotini kufunguliwa mashtaka ya mauji hayo ya Kinyama.

 

Subscribe to eNewsletter